Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Rais wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe Profesa Adolf Mkenda mara baada ya kufika makao makuu ya chama cha skauti yaliyopo upanga jijini dar es salaam leo julai 28,2023 katika hafla fupi ya kuwaaga skauti wanaokwenda Nchini Korea kwenye kusanyiko la 25 la skauti duniani(25th World Scout Jamboree ).
Mhe profesa Adolf Mkenda amewaasa vijana wanaokwenda Nchini Korea kuipeperusha vyema Bendera ya Taifa na kutangaza vivutio vya utalii vya Nchini Tanzania wanapofika huko, Mhe Profesa Mkenda Pia Amepokea mfano wa bima kwa ajili ya safari itakayosaidia skauti hao pindi wawapo safarini wafikapo na kurudi.
Hafla hii ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama cha Skauti Tanzania akiwemo Skauti Mkuu Alt Mhe Rashid Kassim Mchatta,Naibu Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Lt Abuubakar Mtitu, Kamishna Mtendaji wa Chama cha Skauti Tanzania Bi Eline Kitaly pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali na Wazazi,Walimu na Skauti.
MATUKIO KATIKA PICHA
Chanzo cha Habari Tanzania Scouts Association PR-Lab







Ndugu Sabasaba Moshingi Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB bank (kulia) na ndugu Abdulkarim Shah Kamishna Mkuu wa Skauti (kushoto) wakisaini mkataba wa ushirikiano leo tarehe 23 Januari 2018 katika ofisi ya Makao Makuu ya TPB bank, Dar es Salaam[/caption]
Ndugu Sabasaba Moshingi Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB bank akibadilishana mkataba wa mahusiano na ndugu Abdulkarim Shah Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, wa kwanza kushoto ni ndugu Juma Massudi Kamishna Mkuu Msaidizi idara ya Hati na Usajili Chama cha Skauti Tanzania akishuhudia.
Ndugu Sabasaba Moshingi Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB bank na ndugu Abdulkarim Shah Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania wakionyesha mfano wa Kitambulisho cha Skauti pia ni Kadi ya benki.







