Jumamosi, 29 Julai 2023

SKAUTI WANAOSHIRIKI JAMBOREE YA 25 WAAGWA RASMI

 Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Rais wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe Profesa Adolf Mkenda  mara baada ya kufika makao makuu ya chama cha skauti yaliyopo upanga jijini dar es salaam leo julai 28,2023  katika hafla fupi ya kuwaaga skauti  wanaokwenda Nchini Korea kwenye kusanyiko la 25  la skauti duniani(25th World Scout  Jamboree ).

Mhe profesa Adolf Mkenda amewaasa vijana wanaokwenda Nchini Korea kuipeperusha vyema Bendera ya Taifa na kutangaza vivutio vya utalii vya Nchini Tanzania wanapofika huko, Mhe Profesa Mkenda Pia Amepokea mfano wa bima kwa ajili ya safari itakayosaidia skauti hao pindi wawapo safarini wafikapo na kurudi.

Hafla hii ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama cha Skauti Tanzania akiwemo Skauti Mkuu Alt Mhe Rashid Kassim Mchatta,Naibu Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Lt Abuubakar Mtitu, Kamishna Mtendaji wa Chama cha Skauti Tanzania Bi Eline Kitaly pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali na Wazazi,Walimu na Skauti. 


MATUKIO KATIKA PICHA 






Chanzo cha Habari Tanzania Scouts Association PR-Lab

Jumatatu, 5 Februari 2018

Skauti na Vitambulisho

Chama cha Skauti Tanzania baada ya kuendeleza mchakato wa kuwa na mfumo mzuri wa kutunza kumbukumbu za wanachama wake hatimaye sasa wajikomboa.
Mchakato huo ambao ni pamoja na kuwa na kitambulisho au kadi ya mwanachama madhubuti ulianzia tangu mwaka 2015.

[ Ndugu Sabasaba Moshingi Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB bank (kulia) na ndugu Abdulkarim Shah Kamishna Mkuu wa Skauti (kushoto) wakisaini mkataba wa ushirikiano leo tarehe 23 Januari 2018 katika ofisi ya Makao Makuu ya TPB bank, Dar es Salaam[/caption]
Hatimaye leo (23 Januari, 2018) Chama cha Skauti Tanzania kimefanikisha na kuweza kusaini mkataba na Benki ya Posta Tanzania.
Mkataba ambao utawezesha TSA kuwa na “database” ambayo itaweza kuhifadhi kumbukumbu ya mwanachama na kuweza kukusanya ada za mwanachama kwa uhakika zaidi.
“Naweza kusema kuwa ni mfumo wa kwanza kwa Skauti duniani kote, Tanzania tumeonyesha njia bora ya kujua idadi ya wanachama na kwa njia hii” alisema Shah Kamishna Mkuu.

Benki ya Posta wafarijika

Ndugu Sabasaba Moshingi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania alisema benki yao imefarijika sana kwa kushirikiana na Chama cha Skauti Tanzania katika mfumo huu wa kuwezesha mwanachama wa Skauti kuwa na akaunti pamoja na kutumia kadi yake ya benki kama kitambulisho kitakacho weza kuweka kumbukumbu zake.
Ndugu moshing ameyataja baadaadhi ya manufaa yatakayopatikana kwa Skauti kuwa ni kuwezesha TSA kuwa na “database” ya wanachamwa wake, kuwa na kitambulisho cha kisasa chenye kuweka kumbukumbu na pamoja kumwezesha mwanachama kuwa na akaunti yenye kuwezesha kulipia ada yake ya uanachama kwa urahisi zaidi.
TPB bank inajumla ya matawi 68 makubwa na madogo. Ndugu Moshingi alisema wamejipanga kikamilifu na kuweza kufungua “online” kwa njia ya mtandao popote pale utakapokuwa, na huduma zake ni rahisi waweza kutumia mitandao ya simu kuweka akiba yako.
] Ndugu Sabasaba Moshingi Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB bank akibadilishana mkataba wa mahusiano na ndugu Abdulkarim Shah Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania, wa kwanza kushoto ni ndugu Juma Massudi Kamishna Mkuu Msaidizi idara ya Hati na Usajili Chama cha Skauti Tanzania akishuhudia.



Ndugu Sabasaba Moshingi Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB bank na ndugu Abdulkarim Shah Kamishna Mkuu wa Skauti Tanzania wakionyesha mfano wa Kitambulisho cha Skauti pia ni Kadi ya benki.

Balozi Kuahanga naye:

Balozi Nicolaus Kuhanga Mwenyekiti wa Kamati Tendaji Chama cha Skauti Tanzania hakuficha furaha yake na kusema kuwa “ushirikiano huu utaleta maendeleo kwa TSA” aliendelea kusema kuwa mfumo huu utawezesha TSA kuweza kukusanya ada kiukamilifu na bila kificho.

Massudi meno 32 nje

Jambo hili limemfurahisha sana ambalo lipo katika idara yake.

Jumanne, 16 Januari 2018

SKAUTI DAR WATOA FOMU

Chama cha Skauti Mkoa wa Dar es Salaam, kimetangaza kuwepo kwa Mkutano Mkuu Maalum unaotarajiwa kuwepo tarehe za mwisho wa mwezi huu wa Januari 2018.
Akihojiwa ofisini kwake jana 15 Januari 2018 ndugu Abubakar Mtitu Kamishna wa Skauti wa Mkoa wa Dar es Salaam alisema, "Mkoa unatarajia kuwepo na Mkutano Mkuu Maalum ambapo tutaunda Bodi ya Skauti Mkoa pamoja na kuchagua Viongozi wapya wa bodi hiyo"

Nafasi zilizotangazwa kugombea ni Mwenyekiti, Makamo Mwenyekiti ambao watakuwa wawili pamoja na wajumbe wa bodi.

 
Tarehe rasmi ya uchaguzi itatangazwa hivi karibu.
Waweza kujaza fomu hizo za kugombea uongozi kwa njia ya kielektroniki (Online) kwa kubonfya hapa https://tzcentenary2017.wordpress.com/2018/01/16/fomu-ya-uongozi-mkoa-wa-dar-es-salaam/ 

Na kwa habari zaidi za uchaguzi wa Skauti Tanzania kwa ngazi ya Taifa tembelea au bonfya hapa https://tzcentenary2017.wordpress.com

 


Jumamosi, 6 Januari 2018

HURU KUGOMBEA SKAUTI MKUU

Mchakato wa Skauti Mkuu waanza


Chama cha Skauti Tanzania kimetangaza upatikanaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, hii ni desturi ya upatikanaji wa uongozi wa Skauti Tanzania.

Kwa kupitia Mkutano Mkuu Maalum wa Baraza Kuu la Chama cha Skauti Tanzania, ambao ndicho chombo ambacho kinapiga kura na kupata majina 3 yatakayopelekwa kwa Mlezi wa Skauti Tanzania ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuteua Skauti Mkuu.

"Kwa sasa inatarajiwa kuwepo kwa uchaguzi mkuu ambapo tarehe rasmi na eneo litatangazwa" alisema Kamishna Mtendaji wa Skauti Bi. Eline Kitaly

 Kwa sasa Skauti Mkuu wa Skauti ni Bi. Mwantum Mahiza, Kamishna Mkuu wa Skauti ni Ndugu Abdulkarim Shah.

Chama cha Skauti pamoja na kuwa na Makamishna wakuu wa saidizi pia kuna Naibu Kamishna Mkuu ambaye ni ndugu Rashid Mchatta, viongozi wote hao wanamaliza muda wao wa uchaguzi baada ya kupatikana viongozi wapya baada ya uchaguzi na kfuatiwa kuteuliwa kwa Skauti Mkuu na Mlezi wa Skauti (Rais wa nchi)
 Kipenga cha kumtafuta Skauti Mkuu kimepulizwa, mwisho wa kurudisha fomu ni tarehe 15 Januari, 2018 waweza kujaza fomu kielektronik kwa kubonfya hapa ➤ https://tzcentenary2017.wordpress.com/2018/01/06/fomu-ya-uongozi-chama-cha-skauti-tanzania/ pia waweza kupata fomu ya uongozi kwa barua pepe ya: szone2012@live.com au dsmscout@gmail.com
Waweza pia kupakua fomu hii kwa https://web.facebook.com/SCF360